Naibu Waziri Qwaray ataja nafasi ya watumishi utekelezaji Dira ya 2050

NA VERONICA MWAFISI,
Kilwa Lindi

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema Watumishi wa Umma ni miongoni mwa nguzo kuu ya kufanikisha malengo ya taifa hivyo, katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni vema kila mtumishi akaongeza tija, kuboresha utendaji na kuhakikisha mipango ya Serikali inatafsiriwa kwa huduma na matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (katikati) akiteta jambo na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakati wa kikao cha Naibu Waziri huyo na Watumishi wa Umma wa Halmashauri hiyo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.

Mhe. Naibu Waziri Qwaray ameyasema hayo leo tarehe 21 Oktoba, 2026 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

Mhe. Qwaray amesema, lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi hao na kujadili namna bora ya kuimarisha utendaji kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Watumishi wa Umma na kusikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

Naibu Waziri Qwaray alitoa fursa kwa watumishi hao na kusikiliza changamoto na hoja mbalimbali zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yao ambapo baadhi alizifanyia kazi na nyingine alizielekeza kwa Maafisa Utumishi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa haraka.

Vilevile Naibu Waziri Qwaray amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa ili kufikia uchumi wa kipato cha kati cha juu ni wajibu wa Watumishi hao kuongeza kasi ya utendaji, kutumia teknolojia ipasavyo na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma stahiki kwa wakati, kwa haki na bila usumbufu.

Akihitimisha hotuba yake wakati akizungumza na Watumishi hao Mhe. Qwaray amesema, Utumishi wa Umma ni dhamana hivyo, kila mmoja awajibike katika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, taratibu, weledi na maslahi mapana ya Taifa.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakati wa kikao kilichofanyika katika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kikanda, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Mpumbiye Mpumbiye akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko.
Mtumishi wa Umma kutoka Idara ya Kilimo, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bw. Maulid Kikali akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri hiyo wakati wa kikao kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo ikiwemo majengo ya kutolea huduma mbalimbali za afya, shule, nyumba za watumishi, majengo ya utawala pamoja na miundombinu jambo ambalo linawapa ari ya utendaji kazi Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari (kushoto) wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi wa Umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiandika hoja na changamoto zilizokuwa zikiwasilishwa na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakipiga makofi mara baada ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuhitimisha hotuba yake wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here