Makamu wa Rais Ndejembi aipa Wizara ya Viwanda miezi sita kukamilisha Sera ya Biashara Bunifu (Startups)

DAR ES SALAAM- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha ndani ya miezi sita inatengeneza na kukamilisha sera ambayo itajumuisha vitu vingi ambayo itaongoza biashara bunifu (Startups) ili kuratibu kwa kushirikiana na sekta nyingine zenye biashara bunifu mbalimbali.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Biashara Bunifu Tanzania 2026 (Tanzania Startup week 2026) uliofanyika leo Oktoba 19,2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita ni kutengeneza kituo kikubwa kwa ajili ya Startup kukutana na kuendeleza mawazo yao, hivyo ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Viwanda na Biashara kuratibu na kutafuta jengo maalum ambalo litakuwa ni makutano ya startup ili kukuza mawazo hayo.
Aidha, amesema Serikali inaiona biashara bunifu kama eneo linalokua kwa kasi zaidi, hivyo inaendelea kusirikiana na kuwashika mkono na kuwajengea mazingira rafiki wamilki wa biashara changa ili kukuza vipaji na mawazo waliyonayo.

Kwa upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) amesema, wizara hiyo imeendelea kuwa kinara katika kuwawezesha na kuwa sehemu ya kusaidia biashara bunifu ambapo imeweka katika bajeti yake ya 2026/2027 kipengele namba saba

Sambamba na kuanzisha kitengo cha intelijensia ya masoko ambacho kinaenda pamoja na biashara bunifu.
Aidha, Waziri Kapinga ameongeza kuwa, wizara na taasisi zake zimekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wabunifu hasa wanaoanza biashara na wafanyabiashara wote nchini kwa urahisi, kwani taasisi zimeweka mifumo rafiki ili kupatikana kwa urahisi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kukuza Biashara Bunifu, Bw. Zahoro Muhaji amemshukuru Makamu wa Rais kwa kutambua mchango wa taasisi bunifu na kuona umuhimu wa kutambua makampuni hayo, kwani ndio vijana watakaokuwa nguvu kazi ya kesho.
Kongamano linaambatana na maonesho ya wabunifu mbalimbali kwenye sekta mbalimbali ambao wanatoa mchango mkubwa kwenye Sekta ya Mawasiliano, Viwanda na Biashara Nishati na nyinginezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here