Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali leo Oktoba 14, 2026 imeungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kuadhimisha miaka 27 ya kumbukizi ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo amesema, wanaenzi mchango wa Baba wa Taifa katika kuasisi misingi ya umoja, amani na utawala wa sheria.
Kumbukizi hiyo inaadhimishwa leo Oktoba 14, 2026, ikiwa ni miaka 27 tangu kifo chake mwaka 1999, ambapo ni fursa kwa Watanzania kutafakari na kuenzi falsafa zake za Ujamaa na Kujitegemea.
Tags
Baba wa Taifa
Dkt. Ally Possi
Habari
Kumbukizi ya Nyerere
Mwalimu Nyerere
Samia Suluhu Hassan
Taifa