Rais Dkt. Mwinyi avutiwa na huduma za DOC Medical Center Doha

DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Oktoba 9, 2026 ametembelea DOC Medical Center jijini Doha nchini Qatar, kituo cha huduma za afya kinachotoa huduma kupitia idara nane za kitaalamu za kiafya, chini ya mwanzilishi wake na Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Emmanuel Tolessa.
Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amevutiwa na huduma zinazotolewa na kituo hicho, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kupitia Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PSSSF, kwa lengo la kuanzishwa hospitali hii nchini Tanzania.

Kupitia mpango huo wa ushirikiano, DOC Medical Center inatarajiwa kuchangia vifaa tiba, wataalamu wa afya na baadhi ya madaktari, kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya nchini.
Mradi huo unalenga pia kuanzisha huduma za hospitali na famasia, huku kukiwa na matarajio ya kukamilika kabla ya kuanza kwa michuano ya AFCON 2027.

DOC Medical Center ina uzoefu wa kutoa huduma za afya katika matukio makubwa ya kimataifa, ikiwemo michuano ya Kombe la Dunia la FIFA ya mwaka 2022 nchini Qatar.
Rais Dkt. Mwinyi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Qatar leo na anatarajiwa kuelekea Madrid, Uhispania kuendelea na ziara yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here