Rais Dkt. Mwinyi awasili Armenia kumwakilisha Rais Samia katika mkutano wa viongozi wa Dunia kuhusu Bioanuai- COP17

YEREVAN- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Yerevan nchini Armenia leo Oktoba 14, 2026 kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Viongozi wa Dunia kuhusu Bioanuai (Leaders’ Summit on Biodiversity), utakaofanyika Oktoba 16, 2026.
Akiwasili, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi anayewakilisha pia Armenia, Mhe. Fredrick Ibrahim Kibuta pamoja na Naibu Waziri wa Mazingira wa Armenia, Mhe. Ara Mkrtchyan.
Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Leaders for Nature” utawakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na viongozi wa mashirika ya kimataifa kujadili mikakati ya kuhifadhi bioanuai, matumizi endelevu ya rasilimali za kibiolojia, upatikanaji wa fedha na teknolojia, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika uhifadhi wa mazingira.
Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kulinda bioanuai na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za asili kwa maendeleo ya sasa na vizazi vijavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here