TFRA yafanya ziara ya mafunzo Shamba la Sumry mkoani Rukwa kuadhimisha Siku ya Mbolea Duniani

RUKWA-Ikiadhimisha Siku ya Mbolea Duniani, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Joel Laurent, imefanya ziara ya mafunzo katika Shamba la Sumry (Msipazi Farm), kwa lengo la kujifunza teknolojia mpya za kilimo zinazoongeza uzalishaji na tija.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent (kushoto) akisalimiana na Salum Sumry mara baada ya kumtembelea shambani kwake Msipazi Farm, kwa lengo la kujifunza teknolojia mpya za kilimo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mbolea Duniani tarehe 13 Oktoba, 2026.

Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 13, 2026, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa ambapo washiriki wamepata fursa ya kujifunza teknolojia mpya za kilimo cha biashara.

Akizungumza na ujumbe huo, Salum Sumry amesisitiza umuhimu wa kupima afya ya udongo ambapo matokeo yake yatakuongoza kuamua aina ya virutubisho vinavyohitajika na udongo na zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Mamlaka na Mkulima Sumry katika makazi ya mkulima huyo Nkasi mkoani Rukwa tarehe 13 Oktoba, 2026.

Kupitia ziara hiyo, TFRA imesisitiza umuhimu wa wakulima kutumia mbolea bora kwa kuzingatia aina ya zao, hatua ya ukuaji na hali ya udongo, pamoja na matumizi sahihi ya pembejeo ili kuongeza mavuno na kupunguza gharama zisizo za lazima.Meneja wa TFRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Joshua Ng'ondya akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Mamlaka na Mkulima Salum Sumry mara baada ya kuwasili shambani kwake Msipazi Farm, Nkasi Mkoani Rukwa tarehe 13 Oktoba, 2026.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Mamlaka kuimarisha uelewa wa wakulima na wadau kuhusu fursa zilizopo katika tasnia ya mbolea, hususan kwa vijana na wanawake, ili kuchochea ubunifu na maendeleo endelevu ya kilimo nchini.
Mkulima Salum Sumry akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA ,Joel Laurent (hayupo pichani) na watumishi alioambatana nao kwenye ziara ya mafunzo shambani kwake Msipazi Farm Nkasi mkoani Rukwa tarehe 13 Oktoba, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here