Rais Dkt. Mwinyi ziarani Qatar na Hispania

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuondoka nchini leo Oktoba 7, 2026 kuelekea Doha, Qatar kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kufungua fursa mpya za maendeleo kwa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 7, 2026 na Kaimu Mkurugenzi, Mawasiliano, Ikulu Zanzibar, Raqey Mohamed.

Atakapowasili Doha, Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kupokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Habibu Awesi Mohamed.

Katika ratiba yake nchini Qatar, Rais Dkt. Mwinyi atakutana na wawekezaji na wafanyabiashara wa kimataifa kujadili fursa zilizopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hususan katika sekta ya utalii na maeneo mengine ya kimkakati.

Mazungumzo hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano, kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za biashara na ajira.

Baada ya kukamilisha ratiba yake nchini Qatar, Rais Dkt. Mwinyi ataelekea Madrid, Hispania, tarehe 9 Oktoba 2026, ambako atakutana na wadau wa kimataifa katika maeneo ya uwekezaji, maendeleo ya soka na ukuzaji wa vipaji vya vijana, sambamba na kupanua wigo wa ushirikiano wa Zanzibar kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here