Rais Dkt. Mwinyi ashiriki ufunguzi wa COP17 Armenia akimwakilisha Samia

YEREVAN-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi tarehe 15 Oktoba 2026, amehudhuria hafla rasmi ya ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Dunia kuhusu Bioanuai (COP17), uliofanyika katika Kituo cha Michezo na Matamasha cha Karen Demirchyan jijini Yerevan, Armenia.
Rais Dkt. Mwinyi akiwasili kwenye mkutano huo.

Rais Dkt. Mwinyi anashiriki mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo umewakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na wakuu wa ujumbe kutoka nchi mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha juhudi za kimataifa za uhifadhi wa bioanuai na kuharakisha utekelezaji wa malengo ya kuhifadhi na kurejesha mazingira ya asili ifikapo mwaka 2030.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here