Serikali yawataka madereva waliogoma Septemba kuchukua leseni zao

DAR-Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa wito kwa madereva kufuata leseni baada ya kushughulikia mashauri ya madereva hao ambao waliwasilisha malalamiko yao wakati wa changamoto ya madereva wa mabasi iliyotokea Septemba 29, 2026 maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi akizungumza hivi karibuni Ubungo jijini Dar es Salaam.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na Uongozi wa Juu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ukiongozwa na Naibu Waziri, Ayoub Mohammed Mahmoud.

Waziri Katambi amefafanua hatima ya madereva wengine waliobakia ambapo amewataka kufika Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini kwa ajili ya taratibu za kisheria huku akiwataka madereva nchini kutii sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha madhara ya vifo na majeruhi.

Pia, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake katika kuziendea changamoto za madereva ambapo wizara ilipokea maagizo hayo kupitia kwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here