NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia itakayofanyika jijini Bangkok, Thailand kuanzia Oktoba 12 hadi 18, 2026.
Waziri Balozi Omar ambaye pia ni Gavana anayeiwakilisha Tanzania katika IMF na Benki ya Dunia, ataambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba ambaye ni Gavana Mbadala wa Benki ya Dunia, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba ambaye ni Gavana Mbadala wa IMF.
Mikutano hiyo ya mwaka hukutanisha mawaziri wa fedha, magavana wa benki kuu na wataalamu wa uchumi duniani kujadili masuala ya kiuchumi na kifedha duniani.
Tags
Balozi Khamis Mussa Omary
Benki ya Dunia (WB)
Dr Natu El-maamry Mwamba
Gavana Emmanuel Tutuba
Habari
IMF
Kimataifa
Tanzania
Wizara ya Fedha Tanzania
