IRINGA- Baadhi ya wakulima Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamepata elimu kuhusu kanuni kuu nne za matumizi sahihi ya mbolea katika kuchochea uzalishaji tija.

Mwakilishi wa mbolea ya ruzuku TFRA, Kuruthum Manjonjo akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea kwenye Maonesho ya Uwekezaji ya Mufindi (Mufindi Investment Forum and Expo 2026.
Akitoa elimu hiyo kwa wakulima waliotembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwenye Maonesho ya Uwekezaji ya Mufindi (Mufindi Investment Forum and Expo 2026), mwakilishi wa mbolea ya ruzuku, Kuruthum Manjonjo amesema, kupata mbolea kunakwenda sambamba na kuzingatia kanuni za matumizi ya mbolea.
Manjonjo amezitaja kanuni hizo kuwa ni mbolea sahihi, wakati sahihi, kipimo sahihi na mahali sahihi ambazo kwa pamoja zinamhakikishia mkulima uhakika wa mavuno.
Manjonjo amebainisha kuwa, wakulima wanaotumia mbolea bila kuzingatia kanuni hizo huishia kulalamika kuwa mbolea haijafanya kazi, hivyo kuwakumbusha wakulima hao kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajafikiwa na elimu hiyo.
TFRA inashiriki maonesho hayo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwafikia wadau na kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea.
Sambamba na fursa za uwekezaji zilizopo katika mnyororo wa thamani wa mbolea nchini na kuwakumbusha wadau kuzingatia taratibu na sheria zinazosimamia biashara ya mbolea nchini.
Tags
Habari
Habari za Kilimo
Iringa
Kilimo cha Tija
Matumizi ya Mbolea
Mbolea ya Ruzuku
Mufindi Investment Forum 2026
TFRA Tanzania



