TMA yatahadharisha uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa baharini

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi karibu na Visiwa vya Ushelisheli katika umbali wa takribani kilomita 1600 kutoka pwani ya nchi yetu.
TMA imetoa tahadhari kuhusu hali ndogo ya mgandamizo wa hewa katika Bahari ya Hindi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 20, 2026 jijini Dar es Salaam na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwa, mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kuimarika na kuwa Kimbunga katika eneo hilo la Bahari ndani ya kipindi cha siku nne zijazo na mgandamizo huo unaelekea pwani ya nchi yetu.

Aidha, uwepo wake katika Bahari ya Hindi unatarajiwa kuimarisha kiasi mifumo inayosababisha mvua katika maeneo ya ukanda wa pwani ya nchi yetu na maeneo jirani hususani kuanzia Oktoba 24, 2026.
Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi karibu na visiwa vya Ushelisheli.

Aidha, watumiaji wa bahari na jamii kwa ujumla wameshauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

"Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa pamoja na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here