ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema,dua maalum iliyofanyika Kisiwandui leo Oktoba 2, 2026 imelenga kuwaombea na kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki, akiwemo marehemu Mzee Hafidh Ameir Hassan na marehemu Mama Fatma Karume.
Dkt.Mwinyi amesema, marehemu hao walitoa mchango mkubwa kwa vhama, Serikali na jamii kwa ujumla, na kwamba mema waliyoyaacha yataendelea kukumbukwa na kuenziwa.
Aidha, amewashukuru viongozi na wananchi walioshiriki dua hiyo kwa kuonesha heshima, upendo na mshikamano katika kuwaombea marehemu. Dua hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na wananchi.













