Walimu Nkasi waonywa dhidi ya mikopo ya kausha damu, Charles Kasanga ashauri

RUKWA-Walimu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wameonywa dhidi ya mikopo yenye masharti magumu maarufu kama mikopo ya kausha damu, na badala yake wametakiwa kutumia taasisi za kifedha zinazotambulika kisheria ili kuepuka changamoto zinazoweza kuathiri maisha yao na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi wilayani Nkasi, Ndugu Charles Kasanga, wakati wa ziara ya kutembelea walimu waliokumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo Mwalimu Boniface Ndyamukama, ambaye nyumba yake iliteketea kwa moto.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa walimu kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii, nidhamu na uwajibikaji, licha ya changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku.

Pia, amesisitiza walimu kufanya maamuzi sahihi ya kifedha, hususan katika masuala ya mikopo, kwa kuzingatia masharti ya mikopo wanayoichukua na uhalali wa taasisi zinazowakopesha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Nkasi, ndugu Daniel Mpepo, amewataka walimu kuzingatia maadili ya kazi, nidhamu na bidii katika kutekeleza majukumu yao.
Ameeleza kuwa, uwajibikaji wa walimu ni miongoni mwa mambo muhimu yanayochangia kuboresha ufundishaji na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za viongozi wa elimu na CWT wilayani Nkasi za kufuatilia hali za walimu, kuwafariji wale wanaokabiliwa na changamoto na kuwakumbusha wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku, kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya Serikali katika sekta ya elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here