DODOMA- Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera leo Oktoba 19, 2026 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2026.
Ni mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mhe. Simon Songe (Mb).Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Wengine ni Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio, Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti za taasisi hizo.
Tags
Bajeti ya Wizara ya Nishati
Bunge la Tanzania
Dkt. Juma Zuberi Homera
Habari
Habari za Siasa Dodoma
Kamati ya Nishati na Madini
Wizara ya Nishati



