DES MOINES- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani ya mwaka 2026, Bw. Huub Lelieveld, Oktoba 20, 2026 katika ukumbi wa Iowa Events Center, jijini Des Moines nchini Marekani.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani ya mwaka 2026, Bw. Huub Lelieveld, Oktoba 20, 2026 katika ukumbi wa Iowa Events Center jijini Des Moines nchini Marekani.Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amemweleza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha sekta ya kilimo.
Aidha, amemwambia kuwa watafiti wa kilimo nchini Tanzania wanaendelea kujifunza kutokana na kazi zake ikiwemo uhifadhi wavyakula kwa njia za asili.
Bw. Lelieveld ni mwanasayansi kutoka Uholanzi anayejihusisha na masuala ya usalama wa chakula.
Ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2026 na Taasisi ya Tuzo ya Chakula Duniani (World Food Prize Foundation).
Tags
Dr Mwigulu Nchemba
Habari
Habari za Siasa na Kimataifa
Huub Lelieveld
Kimataifa
Sekta ya Kilimo Tanzania
Tuzo ya Chakula Duniani 2026
World Food Prize Foundation


