Soma habari zote muhimu leo Oktoba 21, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, HabariLeo, Majira, Nipashe, Zanzibar Leo, Raia Mwema, Mwanahalisi, Uhuru, Pambazuko, Jamhuri na mengineyo kila siku bila malipo.
MWANANCHI leo Jumatano, Oktoba 21, 2026: KUELEKEA UCHAGUZI CCM 2027: Kumechafuka, kelele tuhuma za rushwa UVCCM. CRDB yabeba tuzo ya Benki Bora 2026. Lissu, ICC, pacha Iran wachuana tuzo ya Sackrov. Ripoti: Sh17 milioni zaibwa kila siku mitandaoni.
HabariLEO toleo Na. 06830, Jumatano Oktoba 21, 2026: Kibano bima ya afya: Mchengerwa aagiza dawa isiyosajiliwa isilipiwe, ataka udhibiti bidhaa ushirikishe TRA, bandari, Uhamiaji. TRA yachunguza biashara ya miwa viwanda vya sukari. Daraja la Pangani ujenzi umefikia asilimia 72.
HabariLEO MICHEZO: Simba, Yanga wote macho makundi - Simba na 15 de Agosto, Yanga na CFFA. Makonda: Tuko vizuri maandalizi AFCON. Misso Misondo ataka matamasha mengi ya Singeli. Octopus mabingwa wa kikapu Mwanza.
DARASA HURU - Dira ya Maendeleo, toleo Na. 101, Jumatano, Oktoba 21-26, 2026: Gazeti limeangazia kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akisisitiza uwajibikaji na usimamizi imara wa mitihani ya Kidato cha Nne, pamoja na wito wa DC Mpogolo kwa KMT kushirikiana na Serikali kuhamasisha usafi.
MAJIRA - Gazeti Huru la Kila Siku, Jumatano 21 Oktoba 2026: Serikali yasisitiza udhibiti wa dawa bandia nchini uimarishwe, ni agizo la Waziri kwa TMDA. Habari nyingine: Tanzania yapiga hatua uzalishaji wa chakula, na BoT, CRDB wapata tuzo kimataifa.MAJIRA MICHEZO: Mashabiki wa Simba SC waruhusiwa dimba la Uhuru kupigana na 15 de Agosto CAFCL, wachezaji wapo kamili gado. Yanga kuishusha mvua ya magoli leo CFFA.
Nipashe leo Jumatano Oktoba 21, 2026: Kauli ya Mchengerwa yawavuruga UVCCM: Waziri adai rushwa imekithiri ndani ya umoja huo, viongozi wake wang'aka wamtaka awataje wahusika. Lissu apenya tatu bora kuwania tuzo kimataifa. Mkosoaji wa Kagame akutwa hana kichwa Uganda.
Michezo Nipashe: MASHABIKI SIMBA SC RUKHSA: Ni katika mechi dhidi ya 15 De Agosto, Yanga kumaliza kazi leo. Libasse kinara wa 'asisti' Bara.
Taifa Tanzania toleo Na. 1559, Jumatano Oktoba 21, 2026: Serikali yalenga dawa za ndani kutosheleza asilimia 80 ya mahitaji, TMDA inaunga mkono lengo hilo. Mwenda: Hakuna biashara itakayofungwa kwa sababu ya kodi. Tuhuma za rushwa UVCCM hali si shwari.
Taifa Tanzania Michezo: Mashabiki Simba wapinga mpango wa kumrejesha Manara, Ahmed Ally atetewa. Miamba ya soka Simba, Yanga SC kazini leo kuwania kufuzu makundi. Ronaldo asimamishwa siku 30 Timu ya Taifa Ureno.
UHURU leo Jumatano Oktoba 21, 2026: Kauli nzito bosi TRA: Awahakikishia wafanyabiashara hakuna biashara itakayofungwa kwa sababu ya kodi. Chatanda ampigia debe Dk. Ndilito ubunge Chamwino. Watatu wadakwa madai wizi betri 40 CT Scan Simiyu.
UHURU Michezo: Yanga, Simba ubabe ubabe: Leo Yanga na Simba zinatarajiwa kuonesha ubabe katika mechi za kwanza CAFCL. SAA 9:00 Alasiri Simba vs 15 Agosto ya Guinea ya Ikweta. Ronaldo ashushiwa rungu Lisbon, Ureno.
Tanzania Leo toleo Na. 001235, Jumatano Oktoba 21, 2026: Samia achochea mjadala Afrika, mafanikio yake yatatumika kujadili uwekezaji viwanda madini, uanzishwaji wa viwanda 24 vya kuchakata madini. CG Mwenda: Hakuna biashara itafungwa kwa sababu ya kodi. Polisi kuanza msako wa silaha haramu Nov. 1.
Spoti Tanzania Leo: CAF yabadili refa wa Simba: Aingia aliyechezesha Kariakoo Dabi. Yanga uwanjani leo Diara, Yao nje. Doumbia amfuata mwalimu wake Pacome. Dube aibuka, aikataa Simba. Kisa kipigo Simba, Mashujaa FC yaingia darasani.
Mwana Spoti - Jumatano Oktoba 21, 2026: Siku ya rekodi: Makocha Simba, Yanga wachimba mkwara. Zinajiandaa kuzoa fedha ndefu CAF. Simba vs Agosto 9:00 Alasiri Uhuru, Yanga vs CFFA 1:00 Usiku Azam Complex. Ronaldo apewa adhabu ya mchongo.
Zanzibar Leo toleo No. 8241, leo Jumatano 21 Oktoba, 2026: Dk. Mwinyi ametimiza ahadi - Waziri Haroun, ni ya upandishaji kima cha mshahara. Dk. Pembe ahimiza ubunifu ZICOO. CCM, CPC vyaahidi kuendeleza ushirikiano. Malipo awamu ya tatu gawio la Sukuk Zanzibar kuanza kesho.
Zanzibar Leo Michezo: Dk. Pembe: Serikali kuendeleza vipaji vya vijana. Bodi ya Ligi yaitisha kikao na klabu za ligi kuu. Simba, Yanga vitani leo CAFCL.
MTANZANIA LEO toleo Na. 215, Jumatano Oktoba 21, 2026: TIRA na wadau wa bima wapeleka tabasamu BMH kwa kuchangia shilingi milioni 221 kusaidia upandikizaji wa figo na uloto. Kamishna Mkuu wa TRA asema hakuna biashara itakayofungwa sababu ya kodi.
MWANANCHI HURU toleo No. 271, Jumatano Oktoba 21, 2026: TIRA na wadau wa bima waipa Hospitali ya Benjamin Mkapa milioni 221 kwa upandikizaji wa uloto kwa watoto wenye selimundu. TRA: Hakuna biashara yoyote itafungwa nchini kisa kodi.
RAIA MZALENDO - Toleo No. 513, Jumatano Oktoba 21, 2026: TIRA yaeleza mtaji wa sekta ya bima umeongezeka maradufu hadi trilioni 2.24, pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA kutembelea kiwanda cha sukari Kilombero na kuahidi kuwawezesha wakulima.
WAMACHINGA - Toleo Na. 5657, Jumatano Oktoba 21, 2026: Polisi watangaza msako wa silaha haramu nchi nzima kuanzia Novemba Mosi, wanaojihusisha wapewe siku 11 kujisalimisha. Waliofariki kwa mauaji Dar kuzikwa siku moja.
WAMACHINGA SPOTI: Yanga: Kesho tunavuka makundi. Rushina ajivunia Simba kurudi Bafana Bafana, Fadlu atajwa kurudi Tanzania, Drogba aitabiria Tanzania AFCON, Nabi atajwa kutua Wydad.
MwanaHabari toleo Na. 3393, leo Jumatano Oktoba 21, 2026: Polisi: Wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishwe kabla ya Oktoba 31, 2026. Tanzania yataja mikakati kukabili uhalifu unaovuka mipaka. Dkt. Pembe aitaka ZiCOO kuwa chachu ya mabadiliko Taasisi za Serikali.
MwanaHabari MICHEZO: Rushine: Simba watanirudisha Bafana Bafana. Mwenda: Nimemalizana na Yanga. Drogba: Tanzania kuna vipaji vya soka. Mwamuzi Simba vs De Agosto huyu hapa. Kocha Muya atamba Championship.




















