Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega ajitambulisha rasmi kwa Jaji Mkuu Masaju

DODOMA-Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega leo tarehe 12 Oktoba, 2026 amekutana na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju kwa lengo la kujitambulisha rasmi baada kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu kushika nafasi hiyo.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega wakifurahia jambo wakati Waziri Ulega alipowasili ofisini kwa Jaji Mkuu leo tarehe 12 Oktoba, 2026 kwa lengo la kujitambulisha.

Akiwa katika mazungumzo mafupi na Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Mhe. Ulega ameeleza ameomba ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu na Sekta ya Haki kwa ujumla.
Mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju, Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Viongozi wengine kutoka Mahakama ya Tanzania na Wizara hiyo. Vilevile, Waziri Ulega ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa miundombinu mizuri ya Majengo sambamba na hatua kubwa iliyopiga katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Kwa upande wake Jaji Mkuu, Mhe. Masaju amemuhakikishia Waziri huyo ushirikiano wa dhati kutoka Mahakama na kusema kwamba ushirikiano kati ya Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria ni takwa la Kikatiba.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimpatia nyaraka mbalimbali za Mahakama Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdalla Hamis Ulega wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 12 Oktoba, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega (wa tatu kushoto). Wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Balozi Baraka Haran Luvanda (wa kwanza kulia) pamoja na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria walioambatana na Waziri.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Amir Mruma (wa pili kulia), Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega (wa pili kushoto), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (wa kwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Balozi Baraka Haran Luvanda (wa kwanza kulia).
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega akitazama picha za Majaji Wakuu ambazo zimebandikwa ofisini kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Masaju. (Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here