Ziara ya Rais Dkt. Mwinyi nchini Qatar, Hispania na Armenia kuleta Mageuzi ya Uwekezaji na Soka Zanzibar

ZANZIBAR- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, ziara zake nchini Qatar, Hispania na Armenia zimefungua fursa za ushirikiano katika uwekezaji, michezo na uhifadhi wa mazingira.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 18, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Oktoba 18, 2026 alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akirejea kutoka ziara hizo.
Amesema, kampuni ya Alfardan ya Qatar imeonesha nia ya kuwekeza Zanzibar, huku makubaliano kati ya Real Madrid Foundation na Unicorn Zanzibar Sports Limited yakilenga kukuza vipaji vya soka kwa vijana na kuimarisha uwezo wa makocha wa ndani.

Aidha, amesema ushiriki wake nchini Armenia umefungua fursa za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika uhifadhi wa mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda rasilimali za bahari.
Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kutekeleza masuala yaliyojadiliwa na makubaliano yaliyofikiwa ili kuhakikisha ushirikiano huo unaleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi na kuchangia maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwasili Oktoba 18, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar baada ya kukamilisha ziara zake nchini Qatar, Hispania na Armenia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here