Maafisa na askari wa vyeo mbalimbali katika mazoezi Songwe leo

Na Mwandishi Wetu| Songwe

AFISA Mnadhimu namba mbili wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Geofrey Munguajuna leo Novemba 28, 2026 amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali mkoani humo katika mazoezi ya kutembea (Route Match).
Matembezi hayo yamefanyika kwa lengo la kuimarisha afya, kuongeza uimara na kujenga utimamu wa mwili na akili kwa askari hao ili kuwawezesha kutekeleza jukumu lla kulinda raia na mali zao kwa ufanisi.
SSP Munguajuna amewahimiza kuzingatia utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kudumisha afya bora, nidhamu, mshikamano na utayari wa kiutendaji katika kutekeleza majukumu ya Jeshi la Polisi, hususan katika kulinda usalama wa raia na mali zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here