Na Mwandishi Wetu| Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Wahid Zahran Nassor kuwa Mthamini Mkuu wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 28, 2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mansura M. Kassim, ambapo uteuzi huo unaanza leo.
Kabla ya uteuzi ndugu Wahid alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Uthamini katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.
