Rais Dkt. Mwinyi apokea Kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa toleo la mwaka 2026

Na Mwandishi Wetu| Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 25 Novemba 2026, amepokea Kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, toleo la mwaka 2026, kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
Kitambulisho hicho kimekabidhiwa na Mkurugenzi wa NIDA Zanzibar, Abdallah Mmanga kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, James Kaji.
Toleo hilo jipya limeboreshwa katika masuala ya usalama na uimara, likilenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi kupitia mfumo jumuishi wa utambulisho wa Taifa, unaowezesha kuunganishwa kwa taarifa na huduma muhimu zikiwemo bima ya afya, leseni ya udereva na hati ya kusafiria kwa matumizi ndani ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here