Na GODFREY NNKO| Dar Es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya muundo wa wizara mbili, uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ili kuimarisha utendaji wa Serikali.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 25, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Dkt. Kusiluka ameeleza kubwa, Mheshimiwa Rais amegawanya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa Wizara mbili (2) ambazo ni; (i) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; na (ii) Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Halihkadhalika, amegawanya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa Wizara mbili (2) ambazo ni: (i) Wizara ya Mifugo; na (ii) Wizara ya Uvuvi.
Uteuzi na uhamisho wa viongozi ni kama ifuatavyo:
A) Mawaziri
(i) Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Balozi Kombo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki;
(ii) Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Kairuki alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari;
(iii) Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Balozi Dkt. Kakurwa alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi;
(iv) Mhe. Hamis Mohamed Mwinjuma (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Uvuvi. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Mwinjuma alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;
(v) Mhe. David Ernest Silinde (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Silinde alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo; na
(vi) Mhe. Beng'i Mazana Issa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
B) Naibu Mawaziri
(i) Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Maghembe alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki;
(ii) Mhe. James Kinyasi Millya (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Millya alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki;
(iii) Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Kamani alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi;
(iv) Mhe. Subira Khamis Mgalu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uvuvi; na
(v) Mhe. Cecilia Daniel Paresso (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo.
C) Makatibu Wakuu
(i) Bi. Agnes Meena ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Meena alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi;
(ii) Prof. Mohammed Ali Sheikh ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi. Kabla ya uteuzi huu, Prof. Sheikh alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya uvuvi;
(iii) Bw. Eliakim Chacha Maswi amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI);
(iv) Bw. Gerson Partinus Msigwa amehamishwa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum;
(v) Bw. Abdallah Hassan Mitawi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mitawi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi;
(vi) Balozi Dkt. Samwel William Shelukindo amepangiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huu, Balozi Dkt. Shelukindo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; na
(vii) Bw. Charles Ngeleja Kadonya amepangiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kadonya alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
D) Naibu Makatibu Wakuu
(i) Balozi Said Shaib Mussa amepangiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huu, Balozi Mussa alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki;
(ii) Dkt. Fabian Magawa Madele amepangiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Madele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya mifugo;
(iii) Bw. Dadi Horace Kolimba ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kolimba alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara - Mikindani;
(iv) Bw. Elijah Greenton Mwandumbya amehamishwa kutoka Wizara ya Fedha kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi; na
(v) Dkt. Amos James Ibrahim ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha anayeshughulikia masuala ya usimamizi wa uchumi. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Ibrahim alikuwa Mhadhiri Mwandamizi, Chuo cha Kodi.
E) Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
(i) Dkt. Ayub Rioba Chacha ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
F) Balozi wa Tanzania nchini Brazil
(i) Balozi Meja Jenerali Wilbert Augustin Ibuge amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Brazil. Kabla ya uteuzi huu, Balozi Meja Jenerali Ibuge alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC).
G) Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
(i) Mhandisi Gilbert Godfried Mwoga ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Mwoga alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Miundombinu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anachukua nafasi ya Mhandisi Victor Hudson Seff ambaye amemaliza muda wake.
H) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)
(i) Bw. Adolf Hyasinth Ndunguru, Katibu Mkuu Mstaafu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Bw. Ndunguru anachukua nafasi ya Bi. Zakhia Hamdani Meghji ambaye amemaliza muda wake.
Aidha, uapisho wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
