Tanzania, China na Zambia zakubaliana kuboresha Reli ya TAZARA kama kichocheo cha uchumi

Na Mwandishi Wetu| Dar Es Salaam

TANZANIA, China na Zambia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa pande tatu na kukuza muunganiko wa kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kupitia uboreshaji na ufufuaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa Mkutano wa pande tatu uliozikutanisha nchi za Tanzania, China na Zambia kujadili kuhusu Uboreshaji wa Reli ya TAZARA na Ujenzi wa Ukanda wa Ustawi uliofanyika Novemba 24, 2026 jijini Dar es Salaam.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe; ujumbe wa China uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Miao Deyu; na ujumbe wa Zambia uliongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi, Mhe. Siazongo Siakalenge.
Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mhe. Maghembe amesema Tanzania inatambua umuhimu wa Reli hiyo katika kuchangia uchumi wa nchi na kwamba Mkutano huo umefanyika wakati muafaka ambapo Tanzania imeendelea kuboresha miundombinu yake ya Bandari, Barabara, Reli na Viwanja vya Ndege ilinkufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.

Aliongeza kusema Mkutano huo umetoa fursa kwa nchi hizo tatu kujadili mikakati ya kuifanya TAZARA kuwa reli ya kisasa, yenye ufanisi na ushindani, itakayochochea biashara, uwekezaji na maendeleo endelevu ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini huku akisisitiza umuhimu wa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo.
Katika majadiliano hayo, nchi hizo zilitambua umuhimu wa kihistoria wa TAZARA kama alama ya urafiki, mshikamano na ushirikiano wa Kusini. Reli hiyo, iliyozinduliwa rasmi mwaka 1976, inaunganisha Bandari ya Dar es Salaam na Zambia na ni kiungo muhimu cha usafirishaji na biashara kwa nchi za ukanda huo.
Zaidi ya kuboresha huduma za usafirishaji, ufufuaji wa TAZARA unalenga kuifanya reli hiyo kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi kwa kurahisisha biashara za mipakani, kupunguza gharama za usafirishaji, kuimarisha mifumo ya ugavi na usafirishaji wa mizigo pamoja na kuvutia uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here