Tanzania na Mauritius kuimarisha ushirikiano katika sekta za kazi na ajira

PORT LOUIS, MAURITIUS- Balozi wa Tanzania nchini Mauritius, mwenye makazi yake mjini Harare, Zimbabwe, Mhe. CP. Suzan S. Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ajira wa Jamhuri ya Mauritius, Mhe. Reza Uteem, katika ofisi za Wizara hiyo nchini Mauritius.
Viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya kazi na ajira, hususan kufungua fursa kwa Watanzania kupata ajira nchini Mauritius katika fani za uuguzi, TEHAMA, huduma za fedha, ufundi na maeneo mengine ambayo wataalamu wake wanapatikana kwa wingi nchini Tanzania.
Aidha, Mhe. Reza Uteem ameeleza utayari wa nchi hiyo kuijumuisha Tanzania katika mpango wa ajira wa nchi hiyo na kuipa kipaumbele katika upatikanaji wa fursa hizo, kwa kuzingatia uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here