Tanzania na Norway zasaini Tamko la Pamoja kuimarisha ushirikiano wa biashara na uchumi

OSLO, NORWAY- Tanzania na Norway zimesaini Tamko la Pamoja Lenye Dhamira ya Kuimarisha Ushirikiano wa Biashara na Uchumi wakati wa Awamu ya Nne ya Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Norway, iliyofanyika jijini Oslo, Norway, tarehe 18 Novemba 2026.
Tamko hilo linatambua biashara, uwekezaji na maendeleo ya sekta binafsi kuwa vichocheo muhimu vya ukuaji wa uchumi endelevu na jumuishi, ubunifu, uundaji wa ajira zenye staha na upanuzi wa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa nchi zote mbili.
Aidha, tamko hilo linadhihirisha dhamira ya pamoja ya Serikali za Tanzania na Norway ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuweka mazingira wezeshi ya kukuza biashara na uwekezaji, kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya Tanzania pamoja na uhusiano wa muda mrefu wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here