Waziri Kombo ataka ushirikiano nchi za Nordic ujikite katika uhawilishaji wa teknolojia na uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania

OSLO, NORWAY- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amezitaka nchi za Nordic kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika uhawilishaji wa teknolojia, uwekezaji na ukuzaji wa ujuzi ili kuongeza thamani ya madini muhimu na kuzalisha ajira.
Mhe. Kombo ameyasema hayo Novemba 19, 2026, jijini Oslo, Norway, wakati wa majadiliano kuhusu Minyororo Endelevu ya Thamani ya Madini ya Kimkakati (Roundtable on Sustainable Critical-Mineral Value Chains), pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Nordic na Afrika.

Akizungumzia sera ya Tanzania kuhusu uongezaji thamani wa madini, Mhe. Kombo amesema: 

Msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko wazi, na tumeuweka katika sheria zetu kwamba rasilimali zinazotoka nchini lazima ziwe zimechakatwa, kama si kikamilifu, basi angalau kwa kiwango cha awali.
Aidha, amebainisha kuwa changamoto kubwa ni upatikanaji wa teknolojia za kisasa za uchakataji wa madini kutokana na kampuni za kimataifa kulinda hataza na teknolojia zao.

Hii ni mojawapo ya changamoto ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo, lakini tunaendelea kutafuta suluhisho kwa kuhakikisha wawekezaji wanapokuja kuwekeza nchini, Watanzania wapatiwe mafunzo ya kitaalamu walau katika walau eneo moja.
Mhe. Kombo ameeleza kuwa nchi za Nordic zina nafasi muhimu ya kuunga mkono juhudi hizo kupitia uwekezaji, teknolojia na utaalamu katika uchimbaji endelevu na wenye uwajibikaji, ili kuhakikisha rasilimali za madini zinachangia maendeleo ya viwanda na ustawi wa wananchi.



Aidha, amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kushirikiana katika kubadilishana ujuzi na teknolojia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here