SAEB EREKAT:TUNATAKA UKOLONI WA ISRAEL DHIDI YA PALESTINA UKOMESHWE MARA MOJA,HATUTAKI MADALALI KWENYE ARDHI YETU

 "Hakuna mzozo kati ya nchi ya UAE na Israel katika ukanda wa Mashariki ya Kati, hakuna mzozo wa nchi ya Oman na Israel, hakuna mzozo wa Sudan na Israeli.Mgogoro uliopo ni mgogoro kati ya Palestina na Israel, ili kuleta amani, usalama na utulivu katika ukanda huu ni muhimu kukomesha ukoloni wa Israel juu ya Wapalestina na kurejesha uhuru wa Palestina ikiwa na mji wake mkuu Yerusalemu Mashariki na katika mipaka ya mwaka 1967,"

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Shirika la Ukombozi la Palestina (PLO), Saeb Erekat ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari nchini hapa.

 Erakat alikuwa akizungumzia juu ya maendeleo ya hivi karibuni ya makubaliano ya nchi ya UAE na Israel (Emirates-Israel Agreement).

Kiongozi huyo amesisitiza kwamba, utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump unatumia kila rasilimali kuizawadia Israel  kwa uhalifu wa kivita dhidi ya Wapalestina na kuongeza kwamba, Mpango wa Amani wa Marekani uitwao Mpango wa Karne (Deal of the Century) ambao unaipa Israel uhuru na udhibiti wa mipaka ya Kimataifa, maji na anga la Palestina ni upuuzi na utani wa karne.

Aidha,katika ujumbe wake kwa Rais Trump, Erekat alimnukuu rais wa zamani wa Marekani, Franklin Roosevelt ambaye alisema kuwa Ikulu ya Marekani ni ofisi ya uwajibikaji wa Kimataifa, kwa sababu mwenye nguvu zaidi, ndiye anayetakiwa kuwajibika zaidi kitu ambacho utawala wa Trump umeshindwa kufanya hivyo.

Pia alibainisha kuwa,Ikulu ya White House inahitaji mamlaka makubwa na sio wakala wa mali au dalali kama Rais Trump.

Mbali na hayo ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kusimama imara na sheria za kimataifa na kuiwajibisha Israeli kwa vikwazo ili kutokomeza ukoloni inaouendeleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news