Serikali mpya ya Yemen yaapishwa, Rais Hadi atoa ya moyoni

Rais Abd Rabu Mansour Hadi wa Yemen amewaapisha wajumbe wa serikali mpya, ambayo iliundwa baada ya kufikiwa makubaliano ya kugawana madaraka yaliyoratibiwa na Saudi Arabia mwaka jana, anaripoti Mwandishi Diramakini (Mashirika).
Viongozi wapya wa Serikali ya Yemen baada ya kuapishwa jana na Rais Abed Rabbo Mansour Hadi mjini Riyadh. (Picha na Saba News Agency/Diramakini).

Serikali hiyo iliyotangazwa wiki iliyopita inajumuisha wanachama kutoka Baraza la Mpito la Kusini linalowakilisha wale wanaotaka kujitenga (STC) kama sehemu ya juhudi za kumaliza vita ya kuwania madaraka baina ya pande mbili. 

Yemen ilitumbukia katika mzozo mbaya tangu mwaka 2014. Wajumbe wa serikali mpya waliapishwa mjini Riyadh ambako Rais Hadi anaishi. 

Rais huyo anayeungwa mkono na Saudia aliitaka serikali hiyo mpya kufanya kazi kwa ushirikiano na kuweka mbele kipaumbele cha kushughulikia uchumi wa nchi ambao umeporomoka. 

Serikali mpya ina wawakilishi sawa kutoka maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Yemen. 

“Ndugu zangu twendeni tukafanye kazi, tunataka ustahimilivu na uimara wa taasisi, kurejesha uchumi, kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa letu, haya mambo ndiyo muhimu kwa sasa.

“Tunahitaji kuuona mjini wa Aden ukiwa huru, vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kutimiza majukumu yake,hatuhitaji vita kuanzia leo, hatutaki umwagaji damu tena,"ameongeza Rais Hadi.

Post a Comment

0 Comments