Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 6,2024

ZANZIBAR-Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahamoud ametangaza kuwapatia wafanyakazi wa ofisi hiyo chai ya asubuhi ikiwa na kitafunwa cha mkate wenye siagi kuanzia leo Jumatatu Mei 06, 2024 ili kupunguza wafanyakazi kuzurura saa za kazi, kuongea na simu mara kwa mara pamoja na kutoka nje kwenda kununua urojo.
RC Ayoub ameyasema hayo Mei 5,2024 wakati akifungua Kampeni ya Amshaamsha Kusini ikiwa na mahususi kwa watumishi wa serikali, lengo likiwa ni kutokomeza uchelewaji kazini, kuzurura muda wa kazi na matumizi ya simu vitu ambavyo amesema haridhishwi navyo, kwani vinachelewesha maendeleo ya wananchi ambapo amesisitiza kuwa gharama zote za chai na vitafunwa zitakuwa zikitoka kwenye mshahara wake yeye mwenyewe.





















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news