Katibu Tawala Mkoa wa Arusha afariki katika ajali akiwa safarini kuelekea Dodoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amefariki kwa ajali iliyotokea eneo la Magugu, Babati mkoani Manyara akiwa safarini kuelekea mkoani Dodoma, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kifo cha Kwitega kimetokea saa 3:50 alasiri ikiwa ni muda mfupi baada ya kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James chenye lengo la kuelimisha umma kuhusu mfumo wa kielektroni wa ukusanyaji wa fedha za umma jijini Arusha jana.

Akithibitisha kutokea kwa kifo cha Kwitega, Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Idd Kimanta alisema gari lake liligongama uso kwa uso na basi la Makala lililokuwa likitokea Babati.

Amesema, baada ya kupata ajali alipelekwa kituo cha Afya cha Magugu, lakini juhudi za madaktari kuokoa maisha yake hazikuweza kufanikiwa. Alisema, taratibu za kusafirisha mwili wake kutoka Kituo cha Afya Magugu kwenda Arusha zilikuwa zikiendelea.

No comments

Powered by Blogger.