Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Julai 29,2022






 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Camilius Wambura, kufanya tathimini ili kuona kama inawezekana kupunguza idadi ya askari wa usalama barabarani ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha kero kwa wananchi.

Kinana ametoa ushauri huo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya mikoa ya Songwe na Mbeya dhidi ya idadi kubwa ya askari wa barabarani ambao wamekuwa wakiwasimamisha mara kwa mara, hivyo kucheleshewesha shughuli za maendeleo.

Malalamiko hayo ya wananchi yaliendelea kuibuka hata kwenye kikao cha ndani cha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ambapo mmoja wa wanachama wa Chama hicho ambaye ni dereva wa magari ya kubeba abiria maarufu kama Costa, kutoa malalamiko yake mbele ya Kinana akidai wamechoka kusimamishwa mara kwa mara na matrafiki na kila wanaposimama wanatozwa Sh. 2000 kwa kila kituo.

Akijibu malalamiko hayo Kinana, alisema kwanza anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IJP Wambura. “Nampongeza Rais kwa kumteua IJP mpya, nina hakika ni IJP mwadilifu, mchapakazi na hodari.

“Lakini ninamuomba na kumshauri atizame wingi wa trafiki mijini, kila baada ya muda mfupi unasimamishwa na trafiki, wenye magari hawaendeshi kwa raha, hivyo nimsihi IJP afanye tathimini kuhusu uwepo wa trafiki wengi kwenye miji yetu, wamekuwa wengi sana kila ukitembea kidogo unasimamishwa, kilometa moja unakuta trafiki.

“Namuomba IJP afanye tathimini watu wapumue, watu biashara zao zinaharibika kwa sababu ya kuambiwa paki pembeni, tunaheshimu umuhimu wa usalama nchini, lakini tunakerwa na kuambiwa paki gari pembeni. Namuomba IJP, naheshimu na natambua uwezo wake mkubwa, lakini afanye tathimini, je, Kuna umuhimu wa kuwa na idadi kubwa ya trafiki barabarani,” Alihoji Kinana.










Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news