Andrew Chenge: Sitakubali maneno yao, nipo imara na nitaendelea kusimama naye

 MBUNGE wa Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu aliyemaliza muda wake,Andrew Chenge amesema kuwa, kuanzia sasa ameyavunja makundi yote yaliyokuwa yakimuunga mkono yeye, badala yake watakuwa ni wamoja ili kumuunga mkono mgombea wa jimbo hilo aliyepitishwa na CCM, Mhandisi Andrea Kundo.


Chenge amewashukuru viongozi wote wa CCM waliompa nafasi ya kuongoza kwa kipindi cha miaka 15 ambayo aliitumia kukomboa jimbo hilo lisiende kwa wapinzani na kwamba ameamua kutoruhusu uwepo wa makundi hayo ili kuepuka anguko la kidemokrasia.

"Niwashukuru sana viongozi wa CCM kwa heshima mliyonipatia tangu 2005, naona kwenye mitandao maneno mengine ya kipuuzi yanasemwa pembeni, nasema kuanzia sasa hakuna kundi la Chenge, kundi letu ni la CCM,"amesema Chenge.

Mwanasiasa huyo Andrew Chenge, amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini ikiwemo Uwaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here