Profesa Mkenda: Kesho Rombo tunaanza kampeni za kisayansi na kistaarabu, kwani siasa ni maendeleo

KATIKA Jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro ambalo lina wapiga kura waliojiandikisha 147,100,wagombea wa vyama sita,ambao walichukua fomu kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,kupeperusha bendera ya vyama vyao kwa nafasi ya ubunge,tayari wamerejesha na kwa sasa wanasubiri uteuzi ili kuanza kwa kampeni, www.diramakini.co.tz

Akizungumza mgombea ubunge  kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)b ya kurejesha fomu,Profesa Adolf Mkenda amesema,watafanya siasa za kistaarabu,kwa kuwa wanaamini siasa ni maendeleo.

"Tunajiandaa kuanza kampeni kesho,kwa taratibu ambazo tutapewa na Tume ya ya Taifa ya Uchaguzi,tutafanya kampeni za kistaarabu,kwani kwetu Rombo,siasa ni maendeleo,siasa si porojo na tutazingatia vipaumbele ambavyo viko kwenye ilani ya chama ikiwemo suala la maji,ambalo limekuwa tatizo sugu Rombo,"amesema Profesa Mkenda.

Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo,Godwin Chacha,akizungumza leo amewataka wagombea ubunge katika jimbo hilo,kueleza sera juu ya watakachofanya kwa wananchi, pindi wakipata nafasi hiyo na kuepuka siasa za kushambuliana na kuchafuana wakati wa kampeni.

"Rombo tutaendelea kuhimiza sheria na taratibu,ili mwisho wa siku, wanarombo, wachague kiongozi wao, wanayempenda, na tutaendesha shughuli zote za uchaguzi kwa demokrasia na vyama vyote tunaamini vitaridhika na kile kitakachotokana na zao la demokrasia, ila niwasisitize wagombea,watumie fursa ya kampeni,kuwaeleza wananchi, watawafanyia nini na kuacha kushambuliana wenyewe kwa wenyewe,"amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo,Dkt. Athuman Kihamia amesma, mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu, ulifanyika kwa amani na utulivu na kutaka uchaguzi usitumike kuvuruga amani iliyopo.

"Rombo hali ya usalama ipo na wagombea wote waliochukua fomu kutoka vyama vyote,wamerejesha kwa amani na utulivu,na ninafurahi kuona vyama vyote vimetii maagizo vizuri na kutekeleza mambo yao kwa amani, naomba uchaguzi usiwe sababu ya kuhatarisha amani yetu,tutambue uchaguzi ni njia tu moja wapo ya kuwapata viongozi kwa njia ya demokrasia,"amesema.

Jimbo la Rombo, ambako, kulizoeleka siasa za vyama viwili,CCM na Chadema,kwa mwaka huu, vitashuhudiwa vyama sita,vikipeperusha bendera katika kampeni,kushawishi wananchi kuchagua mgombea anayetokana na vyama hivyo ambavyo ni, CCM,Chadema,Nccr Mageuzi, ACT Wazalendo, TLP na CUF.

Kwa habari au matangazo (diramakini@gmail.com) www.diramakini.co.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here