Sudan Kusini yasaka mkopo kutibu makovu ya Corona katika uchumi

 SERIKALI ya Sudan Kusini imesema kuwa, imeiomba Benki ya Afrika ya Uingizaji na Usafirishaji Nje Bidhaa (Afreximbank) iipe mkopo nchi hiyo wa kuweza kukabiliana na athari mbaya za virusi vya Corona  (Covid-19). 

Naibu  Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula nchini humo, Lily Albino Akol amesema, mkopo huo utatumika kuisaidia serikali kufanikisha vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kupunguza athari mbaya za ugonjwa wa corona katika sekta ya uchumi nchini humo.

Akol ameyabainisha hayo kupitia mahojiano  yana redio serikali ya Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC).

Naibu huyo amesema,wapo katika hatua za mwisho za kufanikisha kutolewa mkopo huo na kurejea kusema kuwa, mkopo huo utatumika kukabiliana na madhara ya kiuchumi yaliyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 katika nchi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here