RAIS wa zamani wa Jamhuri ya Congo Brazzaville, Pascal Lissouba (88) aliyeitawala nchi hiyo kuanzia mwaka 1992 hadi 1997 amefariki dunia akiwa nchini Ufaransa.
Honore Sayi ambaye ni mbunge na Msemaji wa Chama cha Lissouba cha UPADS alichokiunda mwaka 1991 amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, Lissouba amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa nje.
Pia mtoto wake Jeremie Lissouba ambaye ni mwanasheria, naye amethibitisha kifo hicho.
Baada ya kupoteza madaraka mwaka 1997 kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, rais huyo wa zamani wa Congo Brazzaville alikimbilia Ufaransa mwaka 2004 baada ya kuishi Libreville, Burkina Faso na London kwa muda.
Tags
Kimataifa
