KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), imeeleza dhamira yake ya kuendeleza kilimo cha zabibu mkoani Dodoma pamoja na matarajio yake ya kuingia mikataba ya kununua zabibu moja kwa moja kutoka kwa wakulima wadogo.
Mchango wa TDL
wa sera yake ya kununua malighafi nchini na dhamira ya kukuza sekta ya
kilimo cha zabibu inaenda sambamba na jitihada za Serikali za
kuboresha maisha ya wakulima wadogo na kukuza uchumi wa Tanzania.
Mkulima wa zabibu, Victoria Zablon wa kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma akionja sukari ya zao hilo.
TDL inaamini jitihada za Serikali za kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda zinaweza kufanikiwa ikiwa wakulima wadogo wanawezeshwa kuzalisha malighafi inayohitajiwa na viwanda.
![]() |
| Baadhi ya wakulima wa zao la zabibu Kijiji cha Matumbulu nje ya
Jiji la Dodoma wakiwa na makreti yenye zao hilo baada ya kuvuna tayari
kwa kusafirishwa kupelekwa kiwandani kwa ajili ya uzalishaji wa
vinywaji. |
Meneja Mkuu wa TDL, Devis Deogratius amesema kampuni hiyo kwa sasa inanunua takribani lita milioni 1.2 za mchuzi wa zabibu kwa mwaka kutoka kampuni za CETAWICO na UWAZAMAM, ambazo zinanunua zabibu za wakulima wa ndani ambapo inatumia bilioni 3.3 kwa mwaka.
Mkulima wa zabibu Daniel Ngoima wa Kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma akivuna zao hilo kama alivyokutwa shambani kwake.
