WIZARA YA MALIASILI,UNDP KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA MKAKATI WA KUREJESHA WATALII WENGI TANZANIA

 KATIKA kipindi ambacho ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19) ukiwa unaikabili Dunia, sekta binafsi kwa kushirikiana na sekta ya umma zilifanya kazi kwa pamoja kutengeneza mkakati wa uendeshaji wa shughuli na biashara ya utalii katika kipindi hicho,anaripoti JOHN BERA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Christine Musisi (katikati) pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul,Satbir Singh Hanspaul wakati wa hafla fupi ya makabidhiano wa magari manne ya dharura yaliyotolewa na Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO) jijini Arusha. 

Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Malisiali na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika warsha ya kupokea maoni ya wadau wa utalii katika kuandaa mkakati wa kurejesha sekta ya utalii katika hali yake ya awali baada ya mapambano dhidi ya COVID-19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa ndani ya gari la dharura (ambulence) mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo yatakayo hudumia watalii jijini Arusha.


‘’Tulitengeneza Mkakati huo ambao unaitwa Standard Oparate Procedures ili kuhakikisha kwamba tunaishi na ugonjwa huu kwa maana ya kwamba tusisimamishe shughuli za kuwapokea watalii lakini tujue namna ya kuwapokea watalii ili kusudi watalii wawe salama na watoa huduma wawe salama,’’amesema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akikata utepe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania,Christine Musisi pamoja na viongozi wengine, wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari ya dharura (ambulance) iliyofanyika katika ofisi za Hanspaul jijini Arusha.


Katika Mkakati huo amesema, waliahidi kwamba katika maeneo yao ya utalii wataweka magari ya kubebea wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuandaa maeneo ambayo yatasaidia kutoa huduma pale ambapo ikitokea watalii wamepata tatizo ama watoa huduma wamepata tatizo waweze kuhudumiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Wakati huo huo amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushiriki kuandaa na kuboresha magari ya kubebea wagonjwa kwa kuyabadilisha magari hayo kutoka magari ya kawaida na kuwa magari ya kubebea wagonjwa ambayo yatasaidia kuhudumia watalii watakaopata dharura za maradhi pindi wakiwa katika ziara zao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiipongeza UNDP kwa msaada waliotoa kutengeneza magari yatakayotumika kubeba watalii pindi watakapopatwa na dharura za maradhi, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika kwenye ofisi za Hanspaul, jijini Arusha.


‘’Tunalishukuru Shirika la hili la UNDP limefadhili pamoja na kugharamia magari hayo. Tunashukuru sana kwa kutusaidia na sasa wanatusaidia kazi nyingine maarufu na muhimu sana ambayo ni ya kutengeneza mkakati wa kurejesha hali ya utalii kama ilivyo kuwa awali,"amesema Katibu Mkuu huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news