Yanga yabisha hodi Mahakama ya Kimataifa sakata la Morrison

KLABU ya Yanga imeendelea na msimamo wake wa kukata rufaa kuhusu shauri la Mchezaji Benard Morrison kwa madai bado ana mkataba na klabu hiyo yenye maskani  yake maeneo ya Jangwani, Dar es Salaam, www.diramakini.co.tz

Uamuzi wa klabu hiyo kukata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) inakuja baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kuamuru Morrison ni mchezaji huru.

Mwenyekiti wa Yanga,Dkt.Mshindo Msolla amewaeleza waandishi wa habati leo Dar es Salaam kuwa, wao wanatambua kuwa Morrison bado ana mkataba na Yanga unaoishia Julai 2022.

Pia amesema, rufaa ya mchezaji Morrison kwenda Mahakama ya CAS imekamilika na tayari imetumwa leo ili kuweza kupata kusikilizwa kwa hatua zaidi.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here