BREAKING NEWS: Saed Kubenea adakwa na furushi la fedha

"Mnamo tarehe 5/9/2020, Jeshi la Polisi Tanzania lilimkamata SAED AHMED KUBENEA akiwa katika gari la abiria lenye namba ya usajili T.645 DKR akitokea kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga akielekea Arusha mjini.

"Mara baada ya upekuzi, mtuhumiwa huyo alikutwa, pamoja na vitu vingine,Dola za Marekani Elfu Nane (USD 8000), Shilingi za Kenya Laki Nne Tisini na Moja Elfu Mia Saba (KES 491,700), Shilingi za Kitanzania Elfu Sabini na Moja (TZS 71,000/-), tiketi ya basi la Super Couch lenye namba ya usajili KCP 4230 ya tarehe 05/09/2020 kutoka Nairobi, Kenya kwenda Namanga, ‘Memorandum of Understanding’ kati ya Hali-Halisi (Tanzania) na Buni Media Limited (Kenya), Risiti yamalipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited iliyopo Nairobi, Kenya yenye jina la Kubenea, Saed Ahmedkama mgeni kuanzia tarehe 3/9/2020 hadi 5/9/2020 na Pasi yake ya kusafiria (Passport).
SAED KUBENEA

"Mara baada yakukamatwa, mtuhumiwa alieleza kuwa alifika mkoani Arusha tarehe 2/9/2020 akitokea Dar es Salaam na kufikia katika hoteli iliyopo Arusha mjini.

"Alieleza zaidi kuwa,tarehe 3/9/2020, alienda kulala kwa Kaka yake tarehe 3/9/2020, na tarehe 4/9/2020 alienda Namanga na kupokea fedha taslimu tajwa hapo juu kutoka kwa raia wa Kenya.Hata hivyo, mara baada ya kupitia Ushahidi uliokusanywa nimebaini kuwa:-

"Mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA hakufikia katika hoteli aliyoitaja Arusha mjini,wala kulala kwa Kaka yake kama alivyoeleza.

Mtuhumiwa tajwa alivuka mpaka usio rasmi na kuelekea Nairobi nchini Kenya na kisha kurejea nchini Tanzania bila kutumia mpaka rasmi mnamo tarehe5/9/2020.

"Mtuhumiwa tajwa aliingiza nchini Fedha za Kigeni (foreign currency) bila kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya Kanuni za the Anti-Money Laundering (Cross -Border Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments) Regulations, 2016 zikisomwa pamoja na Kifungu cha 28B(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia Utakasishaji wa Fedha Haramu, Na. 12 ya Mwaka 2006.

"Hivyo, leo tarehe 7/9/2020, mara baada ya kujiridhisha na uwepo wa ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa tajwa, sambamba na misingi ya kikatiba inayoniongoza kama ilivyoanishwa katika Ibara ya 59B(4)(a)hadi (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, nimeidhinisha mashtaka yafuatayo dhidi ya mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA:-a.

"Kuingia nchini Tanzania kinyume na Sheria ya Uhamiaji, Sura ya 54 Marejeo ya mwaka 2016; na b.Kuingiza nchini fedha za Kigeni bila kutoa tamko kinyume na Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani za mwaka 2016,"ameeleza Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania,Biswalo Eutropius Kachele Mganga.








Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news