FC Bayern yatwaa kombe dhidi ya Borussia Dortmund

Hatimaye Klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa German Super Cup dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo wa fainali uliochezwa bila uwepo wa mashabiki uwanjani,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu umemalizika kwa FC Bayern Munich kupata ushindi wa magoli 3-2, magoli ya Bayern yamefungwa na Joshua Kimmich na Thomas Muller.

Borussia Dortmund magoli yao mawili yamefungwa na Brandt na Haaland, ushindi huo sasa unamfanya Thomas Muller aandike rekodi ya kuwa mchezaji wa Kijerumani mwenye mafanikio zaidi baada ya kutwaa taji lake la 27 hadi sasa. "Tumepambana kwa ajili ya kombe, tumepata, Mungu asante,"amesema Joshua Kimmich ambaye amekuwa sehemu ya ushindi huo.

"Ushindi huu kwetu ni heshima kubwa sana, haya ndiyo malengo yetu ya kuyaendea mafanikio," amesema Kocha Hansi Flick baada ya kutwaa ubingwa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news