Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt.Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Mkutano wa 09 wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania unaofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga iliyopo Mkoani Tanga tarehe 15 Disemba 2025.
Akizungumza na Makamanda, Mheshimiwa Rais amelipongeza JWTZ kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha Taifa liko salama wakati wote. Amewahakikishia Makamanda kuwa Serikali itaendelea kuliwezesha JWTZ kwenye kila Nyanja ikiwemo zana, vifaa, Miundombinu na Mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa utulivu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















