Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa ameendelea kuchanja mbuga katika Kanda ya Magharibi huku akijikita zaidi kunadi sera na Ilani ya chama hicho kumuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli, wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho, anaripoti Mwandishi Diramakini...endelea,

SHILINGI BILIONI 5.26 ZATUMIKA KUJENGA BARABARA NGARA
Zaidi ya shilingi bilioni 5.26 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
“Kati ya hizo, shilingi bilioni 1.1 zimetengeneza barabara kwa kiwango cha lami kilomita 4.5 katika makao makuu ya wilaya hii;
Hayo yamesemwa leo Septemba 30, 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Rulenge, katika mikutano uliofanyika kwenye stendi ya Rulenge.
Amesema kiasi kingine cha shilingi bilioni 4.16 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara ikiwemo barabara za Muhweza – Mukarehe, Keza – Nyanzovu, Mukalinzi – Mulonzi, Kibuba – Gwenzaza, Murugwanza - Runzenze (Airstrip), Chivu - Ntobeye – Nyakiziba, Buhororo – Mukididili, Ngara – Kumutana na Buhororo - Ruganzo (Airstrip)
Mheshimiwa Majaliwa ambaye leo anamalizia ziara yake mkoani Kagera ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ngara, Bw. Ndayisaba George Ruhoro na mgombea udiwani wa CCM wa kata ya Rulenge, Bw. John Niyonzima.
Mapema, akiwa njiani kuelekea Ngara akitokea Bukoba mjini, Mheshimiwa Majaliwa alisimamishwa na wakazi wa kata za Nyaishozi (Karagwe) na Kasulo Benaco (Ngara) ambako pia aliwanadi madiwani wa kata hizo. Pia aliwaeleza kwamba barabara ya kutoka Omurushaka hadi Benaco itajengwa kwa kiwango cha lami.
“Kwenye Ilani ya uchaguzi iliyopita ambayo inaisha sasa, barabara hii ilielezwa kwamba itakamilishwa kufanyiwa upembuzi yakinifu, na sasa inaenda kujengwa kwa lami kwa sababu kazi imeshafanyika.”
Pia aliitaja barabara nyingine ya kutoka Bugene – Kasulo (BENACO) yenye urefu wa km. 124 ambayo inatajwa kwenye uk. 75 wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwamba ni miongoni mwa barabara zitakazoanza kujengwa upya kwa kiwango cha lami.
VIJIJI 73 KATI YA 77 MISSENYI VYAPATA UMEME
Wakati huo huo, vijiji 77 kati ya vijiji 73 vya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera vimepelekewa huduma ya umeme na vijiji vinne bado havina umeme.
Hayo yamesemwa jana Septemba 29, 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kassambya, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.
Amevitaja vijiji ambavyo havina umeme na vipo kwenye mpango wa kupelekewa umeme kuwa ni vijiji vya Buchurago, Katano, Kakunyu na Bugango.
Akizungumzia sekta ya mifugo ambayo imetajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 hadi 2025 kuanzia ukurasa 47-52, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeisimamia vizuri sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wanapata manufaa.
“Shilingi milioni 23 zimetumika kukarabati machinjio ya Bunazi hapa Misenyi, pia tumerahisisha uuzaji wa mazao ya mifugo kwa kufuta tozo kero 114 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na kuimarisha masoko ya mazao ya mifugo kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo,” alisema.
Alisema Serikali imepanga kuanzisha vituo vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika mikoa 18 ambayo haina vituo, kuimarisha huduma za tiba za mifugo kwa kuhakikisha kila wilaya ina maabara, kliniki na daktari wa mifugo.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge, Dkt. Florent Kyombo na wagombea udiwani 13 wa CCM wa kata za wilaya hiyo. Mgombea udiwani wa kata ya Kassambya, Bw. Yusuph Jumbe na wenzake sita, wamepita bila kupingwa.
Kuhusu barabara, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 3.57 zilitolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya hiyo zikiwemo barabara za Bukwali-Kashenye-Bushango, Ngorogoro-Kyabugombe, Mabuye –Itara na Ruzinga - Mugongo.

Alizitaja barabara nyingine kuwa ni za Gera – Ishozi – Ishunju, Nyankele – Kilimilire, Mabale–Mwemage-Kyaka, Nyankele-Nyamilembe–Kenyana na Kituntu–Bwengabo. Alisema mwaka 2020/2021, sh. milioni 711.6 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara kwa muda maalum.
HOSPITALI YA WILAYA KARAGWE YAKAMILIKA KWA 98%
Mbali na hayo Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetumia sh. bilioni 1.8 kujenga majengo mbalimbali ya hospitali ya wilaya ya Karagwe ambayo yamekamilika kwa asilimia 98.
Hayo yamesemwa jana Septemba 29, 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kayanga, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Changarawe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera wakati .
Akielezea ujenzi wa vituo vya afya kwenye wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. milioni 900 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya vituo cha afya ambapo kati ya hizo, sh. milioni 500 zimetumika wa majengo ya kituo cha afya cha Kayanga ambapo kituo hicho kimekamilika na kinatoa huduma.
“Shilingi milioni 400 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Nyakayanja na ujenzi umekamilika. Pia shilingi bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi huku fedha za dawa kwa mwezi zilikuwa ni wastani wa shilingi milioni 53,” alisema.
Akielezea uboreshaji wa miundombinu kwenye wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema uk. 74-76 wa Ilani ya uchaguzi ya CCM, unaelezea mpango wa Serikali kuanza ujenzi mpya (km 6,006.04) na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Mugakorongo - Kigarama - Murongo yenye urefu wa km 105.
“Ilani yetu imeenda mbele zaidi na kuelezea mpango wa kukamilisha/kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina (km 7,542.75) barabara za mikoa kadhaa ikiwemo barabara ya Murushaka – Murongo yenye km 125.”
Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe, Bw. Innocent Bashungwa, mgombea udiwani wa kata ya Kayanga, na wagombea wa CCM wa kata za wilaya hiyo.
Alisema, sh. bilioni 1.4 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya kufungua barabara mpya, matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, muda maalum na makalvati. Alisema kati ya hizo, sh. milioni 585 zimetolewa kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi na baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi ni ukarabati katika barabara ya Nyakagoyagoye-Karongo ambao uligharimu sh. milioni 31.
Akielezea ukarabati uliofanywa, alisema sh. milioni 19 zimetumika katika barabara ya Kanyabuleza-Runyaga; sh. milioni 14 zimetumika na katika barabara ya Mato-Karehe; sh. milioni 23 zimetumika katika barabara ya Kihanga - Rwabitembe – Mshabaiguru, sh. milioni 16 zimetumika katika barabara ya Nyakahanga – Kamahungu, sh. milioni 16 zimetumika katika barabara ya Kishoju – Bujuruga na sh. milioni 23 zimetumika katika barabara ya Igurwa-Kibona-Nyakahita.
Alizitaja barabara nyingine zilizofanyiwa ukarabati kuwa ni Katoju-Ihembe – Bisheshe iliyogharimu sh. milioni 98, barabara ya Kanyabuleza Jct-Makabulini iliyotumia sh. milioni 69, barabara ya KDVTC FADECO iliyotumia sh. milioni 73, barabara ya AMRI – CLASIC iliyogharimu sh. milioni 38 na barabara ya Rukore – Chanika iliyotumia sh. milioni 115.
Alisema TARURA ilifanya matengenezo ya madaraja na makalvati katika barabara za Katoju- Rugu - Ruhita (sh. milioni 17), Igurwa-Nyakashozi-Rwentuhe (sh. milioni13), Rukore - Chanika (sh. milioni 12), Rubale - Kibogoizi (sh. milioni 6) na barabara ya Kasheshe - Rubare (sh. milioni 7).
“Shilingi milioni 124 zimetumika kwa ajili ya matengenezo maalum katika barabara za Kajunguti - Rubare - Misha (km. 9), Nyabiyonza-Kafunjo (km. 6), Kibaoni Nyabiyonza Sec - Kakuraijo (km. 3.15), Nyakakika - Kandegesho (km.5), Lukole - Kigarama, Lukoyoyo – Kantabire -Nyakasimbi na Ahamulama – Busecha,” alisema.