Wananchi katika Kata saba kutoka katika tarafa ya Busanda Wilaya ya Geita wanatarajia kumaliza tatizo la vifo vya mama wajawazito pamoja watoto wachanga vilivyo kuwa vinasababishwa na ukosefu wa gari la kubeba wagonjwa kwa ajili ya dharura ili kupelekwa Hospitali vya rufaa ya mkoa wa Geita baada ya kupokea gari lenye thamani vya milioni 32 kutoka Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Geita (GGML),anaripoti Robert Kalokola (Diramakini),Geita.

Simon Shayo Makamu Rais wa Mgodi wa Kuchimba Dhahabu wa Geita (GGML ) kulia akimkabidhi kadi ya gari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka. (Diramakini).
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Dkt. Deo Kisaka ameyasema hayo Septemba 30,2020 wakati wa makabidhiano ya gari la kubeba wagonjwa kutoka GGML kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission kutoka Australia.
Kituo cha afya cha Bukoli kipo umbali wa zaidi ya kilomita 35 kusafiri hadi kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Dkt.Kisaka amesema, gari hilo litaweza kuhudumia kata za Nyamalimbe, Butobela, Nyakagwe, Rwamgasa, Kashishi, Bukoli, Nyakagwe pamoja na Nyaruyeye.
Ameongeza kuwa, kwa wastani wa mama wajawazito, alikuwa anasafiri mama mmoja kila siku kutoka maeneo hayo kwenda hospitali ya wilaya kwa ajili ya matibabu zaidi inapotokea dharura kwa mama anayejifungua au mtoto mchanga.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Bukoli amesema, mwaka jana watoto wawili walifariki duniani kwa kuchelewa kupata usafiri wa kuwawahisha hospitali za rufaa.
Amesema, kupokea gari hilo kutoka GGML itasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga na mama wajawazito wakati wanapopata changamoto za kujifungua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka amesema kuwa tarafa hiyo ya Busanda haikuwa na gari hata moja la kubeba wagonjwa.

Ali Kidwaka (mwenye suti nyeusi katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kulia ni Simon Shayo Makamu Rais wa GGML pamoja na watumishi wa mgodi huo na wataalam wa afya wa Wilaya ya Geita. (Diramakini).
Ameongeza kuwa, GGML imekuwa inasaidia kuimarisha huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.Amesema, tangu mwaka 2017 ameshapokea zaidi ya Bilioni 12.6 fedha kutoka GGML kutokana na fedha za kuhudumia jamii (CSR).
Ametaja kuwa, zahanati 50 zimepauliwa katika halmashauri hiyo,vituo vya afya saba na mwaka 2019 mgodi huo ulitoa vifaa tiba 142 katika vituo vya afya vya Katoro na Bukoli.Kidwaka ameongeza kuwa, GGML imepanga kuchimba kisima kirefu cha maji Kata ya Nyamboge na kutoa magari mengine mawili ya kubeba wagonjwa.
Amefafanua kuwa,GGML pia imeseaidia kuimarisha elimu kwa kujenga vyumba 600 vya madarasa katika halmashauri ya wilaya hiyo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa GGML anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo Endelevu, Simon Shayo amesema kuwa, msaada wa gari hilo umetolewa kwa wakati na utasaidia kutatua changamoto za usafiri kwa wagonjwa mahututi katika kata hiyo ya Bukoli na maeneo jirani.
Ameongeza kuwa,kwa miaka 20 Sasa, GGML kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission wameongeza wigo wa matibabu kwa watoto na watu wazima mkoani Geita ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya midomo sungura na migongo wazi kwa kuwapatia matibabu ya upasuaji bure.
Simon Shayo ameongeza kuwa, mwaka 2004 GGML ilijenga jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya watoa huduma wa afya.
Shayo ametaja baadhi ya miradi ya afya iliyofadhiliwa na GGML kuwa ni kukarabati Hospitali ya Rufaa mkoani Geita,ujenzi wa vituo vya afya katika vijiji vya Nyamalembo,Nyakahongola,Kasota na Kakubilo kwa jumla ya Bilioni 1.8 za kitanzania.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugogo, Zakaria Kishiwa amesema kuwa, wananchi wa kijiji hicho walikuwa wanapata mateso kwa kukosa magari ya kubeba wagonjwa kwa dharura inapotokea wagonjwa wa dharura hasa watoto na mama wajawazito.
Amesema kuwa, wananchi wa kijiji hicho walikuwa wanalazimika kukodi magari ya watu binafsi ili kubebea wagonjwa na kulazimika kulipa kati ya shilingi 80,000 hadi shilingi 100,000.
Zakaria Kishiwa ameomba, Serikali kusaidia kupeleka wataalam wa afya watakaosaidia kutoa huduma ya upasuaji katika kituo hicho cha afya kwa sababu chumba cha upasuaji kilishakamilika pamoja na vifaa tiba vyake.
Pendo Mgawa mwanamke mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa kijiji hicho cha Bugogo Kata ya Bukoli amesema kuwa, mwaka 2009 alinusurika kifo wakati anajifingua kwa kukosa gari la kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Amesema kuwa, alilazimika kukodi gari la mtu binafsi kwa gharama kubwa ya shilingi 100,000 na alikimbizwa hospitali ya wilaya na kufanyiwa upasuaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni Kati ya Halmashauri mbili ambazo zinapokea shilingi Bilioni 9.2 kila mwaka kutoka GGML kwenye mpango wa CSR.Halmashauri nyingine ni Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo fedha hizo zinatumika kwenye elimu,afya,miundombinu ya barabara,masoko ,michezo na miradi ya uzalishaji kwenye jamii mkoani humo.