NEC:Matusi kwa manufaa ya nani?Nadi sera ukishindwa mara moja tutawafungia, tunaongozwa na sheria si mashinikizo

 MKURUGENZI wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Dkt. Wilson Mahera Charles amesema kuwa vyama vinavyotoa matusi kwenye kampeni zao vitachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na vyama hivyo kufungiwa kufanya kampeni,inaripoti DIRAMAKINI.

"Sisi kama NEC tukiona kama kuna chama kinatoa  matusi kwenye kampeni badala ya kunadi sera tutakifungia chama hicho kufanya kampeni hata kama kitaenda Ulaya kulazimika tutakifungia,"amesema.Dkt.Mahera ametoa kauli hiyo jijini Dar es wakati akifungua mkutano  wa siku moja kwa watoa huduma za habari mitandaoni. 

Amesema, katika kipindi hiki kuna baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa lugha za matusi na za uzalilishaji jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uchaguzi. 

Amesema japo hiki ni kipindi cha kampeni, lakini sheria nyingine zote zinaendelea kufanya kazi hivyo hawatasita kuchukua hatua. 

Aidha, amewapongeza watoa huduma mitandaoni kwa kutoa taarifa za uchaguzi na kwamba  watoa huduma mitandaoni ni wadau muhimu wa uchaguzi na kuwataka kuhakikisha utoaji taarifa unakuwa uendelevu kudumisha amani. 

Amevitaka vyombo hivyo kuendelea kuhamasisha watanzania ili wajitokeze siku ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura na kwamba ushirikiano na vyombo hivyo utafanikisha mchakato mzima wa uchaguzi. 

Aidha, amevitaka vyombo hivyo kutoa taarifa sahihi na kwa wakati na pia kutotoa taarifa kwa upendeleo wa kuangalia vyama na badala yake watende haki kwa wagombea wa vyama vyote. 

Amesema kuwa, NEC haitafanya kazi kwa mashinikizo ya matafaifa ya nje na kuitaka vyama hivyo kuzingatia sheria. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news