Rais Magufuli, Museveni watiliana saini mkataba wa makubaliano wa kuanza rasmi Mradi wa Bomba la Mafuta

RAIS wa Jamhuri ya Uganda,Yoweri Museveni leo Septemba 13, 2020 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini ambapo ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kukamilisha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na maafisa wa Uganda baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuondoka kurejea nyumbani, baada ya kutia saini waraka wa pamoja kuanza haraka Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Utiaji saini huo umefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita ambapo waheshimiwa marais hao pia wametia saini waraka wa pamoja wa kuagiza kuanza haraka kwa utekelezaji wa mradi huo.

Kikundi cha ngoma ya Rubirigi kikitumbuiza wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni (hawapo pichani) wakitia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakiwemo mawaziri, wanasheria wakuu wa Serikali,wakuu wa mikoa,makatibu wakuu, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,viongozi na wataalamu wa taasisi mbalimbali za Serikali na viongozi wa vyama vya siasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Uganda,Yoweri Museveni wakati akiondoka kurejea nyumbani baada ya kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani amesema bomba litakalojengwa litakuwa na urefu wa kilomita 1,445 ambapo kilomita 1,149 kati yake zinapita nchini Tanzania, litapita katika mikoa nane, wilaya 24 na vijiji 280 hapa nchini, litakuwa na uwezo wa kupitisha mapipa 216,000 kwa siku, litazalisha ajira 10,000 na kwamba kwa miaka 25 ya mradi huo Tanzania itapata mapato ya kiasi cha shilingi trilioni 7.5.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni akimsindikiza mgeni wake anayeagana na mawaziri wa Tanzania wakati akiondoka kurejea nyumbani baada ya kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Prof. Adelardus Kilangi amesoma maelekezo ya pamoja yaliyotolewa na kutiwa saini na waheshimiwa marais ambapo wameelekeza kuwa kila nchi ichukue hatua za haraka ili kutia saini mkataba kati ya nchi husika na kampuni zinazotekeleza mradi huo, kila nchi ianze kwa haraka mashauriano ili kusaini mikataba midogo inayohusika katika mradi huo na pia kila nchi ichukue hatua ili kuwezesha utekelezaji wa haraka wa mradi huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akimshukuru kwa hotuba nzuri Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni mara baada ya kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Katika hotuba yake Rais Magufuli amempongeza na kumshukuru Rais Museveni kwa kuchukua hatua madhubuti za kutafuta mafuta nchini mwake, kukubali bomba lipitishwe nchini Tanzania na pia kuridhia asilimia 60 ya faida ichukuliwe na Tanzania ambako bomba linapita kwa zaidi ya asilimia 70 huku Uganda ikichukua faida kwa asilimia 40.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni wakitia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi
iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Rais Magufuli amesema kutekelezwa kwa mradi huo ni ushindi mkubwa wa kiuchumi kwa Uganda na Tanzania pamoja na ukanda wote wa Afrika Mashariki na ameahidi kuwa Tanzania itasimamia masuala yote yaliyobaki ili utekelezaji uanze haraka kwa manufaa ya Watanzania na Waganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt. John Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni wakishuhudia mawaziri wa Nishati wa nchi zao Mary Goretti Kitutu wa Uganda na Dkt.Medard Kalemani wa Tanzania wakitia saini mkataba wa kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Rais Magufuli ameeleza kuwa kutekelezwa kwa mradi huo kutarahisisha upelekaji wa gesi ya Tanzania nchini Uganda kupitia njia hiyo hiyo na pia kutarahisisha usafirishaji wa mafuta yanayotafutwa katika mbuga ya Wembele nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni alipowasili kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Kwa upande wake, Rais Museveni ameelezea kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na amebainisha kuwa kwa sasa jambo muhimu ni kuanza utekelezaji wa mradi ili wananchi waanze kuona manufaa yake badala ya kupoteza muda mwingi zaidi katika majadiliano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda,Yoweri Museveni alipowasili kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza
kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.


Rais Museveni amesema, utafiti uliofanywa katika asilimia 40 ya bonde la mto Albert huko Hoima nchini Uganda umebaini kuwepo kwa mapipa bilioni 6.5 ya mafuta ghafi na kwamba zipo dalili njema kuwa asilimia 60 za eneo ambalo halijatafitiwa pia kuna mafuta na kwamba Uganda inatarajia kupata mafuta mengine katika ukanda wa Kadamu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni alipowasili kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni akizungumza baada ya kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akizungumza mbele ya mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Uganda,Yoweri Museveni mara baada ya kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza
kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Uganda,Yoweri Museveni wakati wa sherehe fupi ya kutia saini waraka wa pamoja unaoagiza kuanza haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato.

Rais Museveni amesimulia kuwa, baada ya kubaini kuwa wataalamu wa mataifa ya nje walikuwa wakimyumbisha katika mpango wake wa kupata mafuta nchini Uganda, aliamua kuchukua hatua za kuwasomesha vijana wa Uganda na baadaye vijana hao wakafanya utafiti na kisha kupata mafuta ambayo leo yamefikia hatua ya kuchimbwa.

Pia ametoa wito kwa wananchi wa Tanzania na Uganda kuamka na kuchapa kazi za uzalishaji mali kwa maendeleo badala ya kuishia kuzalisha kwa kujikimu,baada ya hatua hiyo Rais Museveni amerejea nchini Uganda. (Picha na Ikulu/Diramakini).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news