Maalim Seif Sharif Hamad ataja vipaumbele vyake akipewa ridhaa Oktoba 28

CHAMA cha ACT-Wazalendo leo Septemba 13, 2020 kimezindua kampeni ya Urais wa Zanzibar ambapo Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe ameowaongoza maelfu ya wanachama, wapenzi na wakazi wa Zanzibar kuomba kura kwa ajili ya mgombea wao, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Miongoni mwa mambo ambayo wamesema wakipewa ridhaa ya kuwaongoza wananchi Zanzibar wataanza kuyatekeleza mara moja ni pamoja na kurejesha mamlaka kwa Serikali ya Zanzibar katika kutunga na kutekeleza sera muhimu za uchumi ikiwemo kodi ya mapato kwa makampuni.

Pia uwezo wa ushirikiano wa kimataifa kwa mambo yasiyo ya Muungano na uwekezaji kutoka nje ili Zanzibar iweze kujenga uchumi imara unaoendana na mazingira yake.

Aidha, wamesema wakishinda nafasi hiyo ya urais, uwakilishi na madiwani watahakikisha wanalipa malimbikizo yote ya haki za mapato ya Zanzibar kutokana na mapato ya ziada ya Muungano kama ilivyochambuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha. Kwa habari mpya hapa.

ACT-Wazalendo kimesema Serikali yao kila mwaka, kwa miaka mitano, Serikali ya Muungano itailipa Serikali ya Zanzibar shilingi bilioni 66.

Sambamba na kutekeleza mamlaka ya kikatiba ya Zanzibar katika mashirika ya Kimataifa ambayo yanashughulika na masuala yasiyo ya Muungano kwa kuifanya Zanzibar kuwa mwanachama wa mashirika ya Kimataifa kama vile FIFA, WHO, UNESCO, UNICEF na mengine mengi.
Uzinduzi huo ambao ulifanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti katika Kisiwa cha Unguja jijini Zanzibar uliwakutanisha maelfu ya wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news