YANGA SC: Tupo imara, ole wao ambao watazifanyia hujuma jezi mpya

KLABU ya Yanga  SC leo Septemba 11, 2020 imezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020/21, uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya uzinduzi huo mashabiki wengi pamoja na wadau walijitokeza kushuhudia walianza kuzinunua hapo hapo.

Fredrick Mwakalebela ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC amesema kuwa,wale ambao watachakachua jezi hizo watachukuliwa hatua mara moja.

Amesema, msimu huu wameandaa kikosi kazi ambacho kinafanya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuhakikisha hakuna ambaye anafanya hujuma katika jezi zao.

 ”Tumekuwa timu ya kwanza kuzindua duka la vifaa vya Yanga SC pamoja na jezi nzuri na yenye ubora, hivyo tupo imara katika kila idara na tunaamini kwamba tutafanya mengi makubwa,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news