Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi atoa maelekezo kwa watumishi wapya

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amewataka watumishi wapya kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kuleta matokeo chanya kwa Serikali,anaripoti LORIETHA LAURENCE-WHUSM.

Dkt.Abbasi ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyotolewa kwa watumishi hao wa kada ya habari ikiwa ni tararibu ambazo hufanya kwa kila mwajiriwa mpya wa Serikali.

“Natoa rai kwenu hakikisheni mnayaishi na kuyatenda yale yote mliyofundishwa na wataalamu ili muweze kutekeleza majukumu na kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali,”ameema Dkt.Abbasi.

Ameongeza kuwa, wizara hiyo inasimamia sekta za burudani ambazo huwaleta wananchi kwa pamoja na umoja bila kujali kabila wala dini ambapo ni 'soft power' muhimu ya nchi hivyo watumishi hao walisisitizwa kuzingatia utaalamu, weledi na ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuleta manufaa kwa Serikali na wananchi kwa ujumla. 

Dkt.Abbasi pia amewataka watumishi hao kuwa mabalozi wazuri katika kutunza siri za Serikali, kufanya kazi kwa ushirikiano, kuwa na mahusiano mazuri na watumishi wengine, kuweka malengo katika utendaji wao wa kazi ndani na nje ya utumishi wa umma ili kuwezesha kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara.

Mafunzo hayo yalihitimishwa kwa kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma ambacho waliapa mbele ya mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Hassan Abbasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news