Maalim Seif:Huduma za afya zitakuwa bure, Zanzibar itakuwa kitovu cha uchumi Afrika

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza kuwa, anatarajia iwapo atapewa ridhaa na wananchi kuwa Rais wa Zanzibar, Serikali yake itatoa huduma bora za afya na bure kwa wananchi wote wa Zanzibar, anaripoti Talib Ussi (Diramakini).

Maalim Seif ameyaeleza hayo huko Mtambwe Makoengeni Wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake kwa upande wa Zanzibar. 

Mgombea wa Urais Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa JiMbo la Mtambwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba mkutan uliofanyika Makoengeni Mtambwe Kusini. (Diramakini).

Ameeleza kuwa, afya ndio kila kitu katika maisha ya binadamu na kusema kuwa bila ya afya hakuna ambacho mtu anaweza kufanya.

“Kama watu wako hawana afya hata uzalishaji utashukana juhudi zote za maendeleo haziwezi kufanikiwa kwa hiyo tunakusudia kutoa huduma bora na zikiwa bure kabisa,”amesema Maalim Seif.

Amesema, atahakikisha hospitali zote zinakuwa na vifaa, watalamu, madaktari bora na stahiki zote za madaktari ili kushawishika kutoa huduma bora na kwa wakati. “Nitahakikisha dawa za aina zote na huduma muhimu zinapatikana katika hospital zote Zanzibar,”amesema Maalim Seeif.

Maalim Seif amesema, kila hospitali itakuwa na madaktari wenye sifa, odari na madawa ya aina zote kwa wananchi Zanzibar.

Sambamba na hilo kila daktari anayefanya kazi katika hospitali atatakiwa kuwa na ujuzi wa kutosha kwa sababu anashughulikia maisha na miili ya watu.

“Tutakuwa na madaktari wazuri walisomeshwa na kuwa na sifa bora ambao watatakiwa kufuata maadili ya kazi zao,"amesema Maalim Seif ambapo amesema kuwa, yeyote atakayekwenda kinyume na maadili atachukuliwa hatua ikiwemo kuondolewa kazini.

“Leo mzazi anafika hospitali na anatafunika uzazi, lakini unamkuta mkunga hata habari hana, sisi wakunga hao hatuwataki kabisa, tunataka wakunga wenye kujali maisha ya watu,"amesema huku akiongeza kuwa, anataka kuifanya sekta ya Afya kuwa kivutio cha Utalii Zanzibar kwa kile alichokieleza kutokana huduma zitakazotolewa watalii wengi wapate hamu ya kutembelea Visiwa vya Zanzibar.

Amesema kuwa, wananchi wa Zanzibar watapata matibabu bure kwa aina yoyote kwa sababu Wazanzibar ni haki yao kikatiba ila wageni watalipishwa. Kwa upande wa majengo Maalim Seif almeeleza kuwa, Serikali itakayongozwa na ACT Wazalendo itajenga majengo yenye kiwango na ubora mkubwa na usafi wenye kuvutia.

Kwa upande mwingine Maalim Seif anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikuu cha mawasilino kwa nchi za Afrika ili nchi zote zinazozunguka Zanzibar wapate huduma zote wanazozitaka.

“Huduma zote zitapatikana Zanzibar na nchi yoyote itakayoamuwa kupitisha mizigo yao watakuwa huru,”amesema Maalim Seif huku akiongeza kuwa, nchi jirani kama zinachimba mafuta meshine zao zitatoka Zanzibar na baadae kuzipeleka katika nchi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news